VALENCIA,CELTIC NA SHAKTAR ZAFANYA KWELI UEFA

Celtic wakicheza
katika uwanja wao waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Malmö.
Mabao ya Celtic yakifungwa na leigh Griffiths aliyefunga mabao mawili na
Nir Bitton , huku ya Malmo yakifungwa na Jo Berget aliyefunga mabao
mawili pia.
Valencia wakiwa nyumbani Mestalla wamewachapa As
Monaco kwa mabao 3-1,Daniel Parejo, Rodrigo na Sofiane wakifunga mabao
ya wenyeji huku bao la Monaco likiweka kambani na Mario Pasalic
Matokeo mengine ya michezo hiyo
Basel 2 – 2 Maccabi Tel Aviv
Rapid Vienna 0 – 1 Shakhtar Donetsk
Skenderbeu Korce 1 – 2 Dinamo Zagreb
Maoni
Chapisha Maoni