MAN UTD YAUA 3 UEFA

Memphis Depay ameonesha ubora wake hapo jana baada ya kuisaidia klabu yake ya Manchester united kuibuka kidedea cha mabao 3-1 dhidi ya Club Brugge huku yeyeakitupia jumala ya mabao mawili.

Katika mtanange huo ulioanza kwa kasi ya ajabu kiungo wa manchester united Michael Carrick alijikuta akijifunga mapema tu mnamo dakika ya 8 alipokuwa akijaribu kuokoa.
Depay alianza kwa kulikomboa goli hilo mnano dakika ya 13 na kuongeza jingine dakika ya 43 zikiwa zimesalia dakika mbili waende mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku manchester wakionekena kubadilika kwa kiasi kikubwa na kupelekea kupata bao la tatu mnamo dakika za nyongeza (90+4) likifungwa na Maruani Fellain.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza ya michuano ya klabu bingwa Ulaya UEFA ambapo man utd walikuwa nyumbani ambapo Mephis Depay alikuwa mchezaji bora(man of the match).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii