MAN UTD YAPIGA 4-0, LVG AMPONGEZA ROONEY

 Louis van Gaal amemsifia Wayne Rooney kwa uwezo wake baada ya straika huyo kufunga hat-trick katika ushindi wa Manchester United wa 4-0 dhidi ya Club
Brugge.

Straika huyo wa England katika mechi 10 alishindwa kupata hata goli moja lakini jana alizama nyavuni mara tatu na kupelekea timu yake ikiwa ugenini kuibuka kidedea na kusonga mbele kwa wastani wa magoli 7-1.
Van Gaal anaamini amefanya kazi kubwa kuhakikisha anamrudisha  Rooney katika hali ya kujiamini kutokana na maneno ya watu na mashabiki yaliyokuwa yakimvunja moyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii