MAN CITY YAPAA KILELENI EPL

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kunyakua point tatu hii usiku wa leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Brom Albion. 
Manchester City ikiwa na nyota wake wote
muhimu ilianza mchezo kwa kasi huku ikiwapeleka wapinzani wao mpera mpera na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Man City walikuwa wakiongoza 2-0 yote mawili yakifungwa na Yaya Toure dakika ya 9 na 24.
Wapinzani wao walionekena kuzidiwa kila sekta kwani hata kilipoanza kipindi cha pili West brom waliendelea kuhaha kutfuta mpira huku wakijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza mara tu wakiupata mpira lakini haya kuzaa matunda.
Alikuwa ni Vicent Kompany nahodha wa Man city ikiwa ni dakika ya 59 alipokamilisha kalamu ya mabao matatu, ushindi ambao ni mnono kwa Man city waliokuwa ugenini katika uwanja wa The Haw thorns.
Baada ya ushindi huo Man city inapaa hadi kileleni na kuishusha ambayo ilikuwa ikiongoza kabla ya mhezo wa leo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii