REAL MADRID KUWAVAA JUVENTUS HII LEO UEFA (PICHA)

Ni katika mtanange mkali utakao choma nyasi za Santiago Bernabeu hii leo13Mei 2015 majira ya 9:45 usiku ambapo wenyeji Real Madrid watakuwa wanawakaribisha (vibibi vya Turin) Juventus katika mchezo wa marudiano wa nusu
Real Madrid host Juve in the second leg of the Champions League semi-finals
fainali UEFA.

Ikumbukwe kuwa katika mtanange wa kwanza uliofanyika huko Italy Juventus iliibuka kidedea kwa kuilaza Madrid 2-1.

Real Madrid watakutana na mchezo mwingine mkali wakati baada ya kuambulia sare ya 2-2 katika mchezo wa La Liga wakiwa nyumbani dhidi ya Valencia, na kufanya tofauti ya pointi nne dhidi ya vinara Barcelona zikiwa zimebaki mechi mbili tu.
Katika mpambano wa leo kiungo wa Juve Paul Pogba anatarajiwa kurejea uwanjani kuwavaa Real Madrid hii ni kutokana na majeraha aliyokuwa nayo yaliyo mfanya asicheze mechi ile ya kwanza.
Pia naye Mshambuliaji wa Real Karim Benzema anatarajiwa kurejea uwanjani hii leo baada ya kuwa nje ya uwanja takribani majuma matatu.
Juventus ambao wamefanikiwa kuishinda Real katika michuano hiyo mara tatu kati ya mipambano minne huku  Real Madrid wakishinda mara moja tu mnamo mwaka 1998 katika fainali.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii