Karibu upate habari za michezo ya aina zote kwa haraka na uhakika. Utapata habari za soka, mpira wa kikapu, Tennis, mpira wa pete, masumbwi, mashindano ya magari, riadha na michezo mingine. Hapa utapata matokeo ya mechi mbalimbali, taarifa za wachezaji na timu zao.
JUVE SASA USO KWA USO NA BARCA
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Juventus watakutana na Barcelona katika fainali ya michuano ya UEFA baada ya goli la Alvaro Morata hapo jana kuwapeleka mbele kwa jumla ya magoli 3-2 ukiwa ni ushindi dhidi ya Real Madrid ambao walikuwa wenyeji pale Bernabeu.
Waitalia hao walikuja nyuma baada ya goli la kuongoza la Cristiano Ronaldo mnamo dakika ya 23 kwa penati na kuwafanya Real kuwa kifuambele hadi mapumziko.
Katika mpambano huo wa jana ambapo ulimalizika kwa sare ya 1-1 uliwanyima nafasi Real kutokana na mechi ya kwanza kufungwa 2-1.
Chelsea imefanikiwa kumsajili Michy Batshuayi Michy Batshuayi amefanikiwa kujiunga na Chelsea baada ya kukamilika kwa vipimo vya afya huko Bordeaux, chanzo cha Sky kimeripoti
Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Didier Drogba alikataa kuichezea Montreal Impact baada ya kuambiwa hataanzishwa dhidi ya Toronto ,kulingana na kocha Mauro Biello
Maoni
Chapisha Maoni