YANGA YATINGA KILELENI

 Klabu ya Yanga ali maarufu wanajangwani leo imefanikiwa kutinga kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kufanikiwa kuibuka kidedea cha 1-0  mbele ya Wagosi wa kaya Coastal Unioni katika uwanja wa
Mkwakwani Tanga.

Bao lililoiletea ushindi Yanga ni bao la Nahodha Nadri Haroub Ali "Cannavaro" mapema kabisa katika kipindi cha kwanza mnamo dakika ya 12 ya mchezo.




Baada ya ushindi wa leo Yanga inajikita kileleni Mwa ligi kuu ya Vodakom ikiwa na jumla ya pointi 22 baada ya mechi 12 hivyo imeishusha Azam iliyokuwa kileleni ambayo inapointi 21.

Mechi ya leo ilianza kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu lakini uzembe wa mabeki wa Coastal Unioni umewaponza kwani goli alilolifunga Cannavaro lilitokana na mpira uliorushwa na Mbuyu Twite Kpah Sherman akaugonga kichwa kabla ya Cannavaro naye kumalizia kwa kichwa.

 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao


Kikosi cha wanajangwani 


Nembo ya Klabu ya YANGA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii