USAJILI ULIOFANYWA NA CHELSEA KATIKA DIRISHA DOGO

Katika usajili wa dirisha dogo uliokamilika februari 2 mwaka huu vilabu mbali mbali vimewauza wachezaji na kuwanunua wengine ambao hata hawakutarajiwa kuuzwa au kusajiliwa na mashabiki wa
vilabu hivyo.

Kwa upande wa klabu ya Chelsea katika usajili huo wa dirisha dogo imemuuza mchezaji mmoja Andre Schule ambaye ameelekea Wolfsburg kwa dau la Euro 28 milioni. 

Mchezaji mwingine ambaye ameondoka Chelsea ni Mohamed Salah ambaye ameelekea Fiorentina kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu kama dili la kupunguza ada ya kumnunua Juan Cuadrado.

Chelsea pia imefanikiwa kumnunua winga matata kutoka Fiorentina Juan Cuadrado kwa dau la Euro 25milioni baada ya kupunguziwa kutokana na kumpeleka Salah kwa mkopo kwani mwanzoni ilikuwa Euro33milioni.

Andre Schule alipokuwa Chelsea kabla ya kuondoka katika dirisha dogo kuelekea Wolfsburg


Mohamed Salah akiwa Chelsea kabla ya kuelekea Fiorentina kwa mkopo


Juani Cuadrado akiwa Fiorentina kabla ya kutimkia Chelsea msimu huu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii