SIMBA YAAMBULIA SARE MKWAKWANI TANGA

Klabu ya Simba kwa mara nyingine tena imeweza kuambulia sare ya 0-0 mbele ya wenyeji wao Coastal Union katika mpambano wa ligi kuu bara uliochezwa mapema hii leo majira ya saa 10:00 jion
i.

Mpambano kwa ujumla ulikuwa wa vuta ni kuvute japo haukuwa na kashi kashi sana kama tulivyo zoea Simba au Yanga wakienda Mkwakwani.

Timu zote mbili zilijitahidi kutoa mashambuli kwa kutumia mipira ya katikati na pembeni lakini mabeki wa timu hizo waliweza kuwadhibiti vilivyo washambuliaji wa timu zote.

Katika safu ya ushambuliaji kwa upande wa Simba alikuwa ni Elias Maguli Pamoja na Dan Sserrunkuma huku Okwi akicheza kama winga wa kushoto, upande wa wagosi wa kaya alikuwa ni Iker Obinna na Rama Salim.

Kutokana na matokeo hayo Costal unioni inatimiza pointi 18 huku Simba ikitimiza pointi 17.

Kocha wa Simba Msebia Prujim akiwa haamini kinachotokea uwanjani


Kikosi cha Simba kilicho cheza hii leo kule Mkwakwani


Nembo ya klabu ya Simba

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii