MATOKEO LIGI KUU UINGEREZA HAYA HAPA (PICHA)

  • Baada ya baadhi ya timu takribani 12 kumaliza mechi zake hivi punde na hapa nakuletea matokeo yote waliofunga na kila timu katika msimamo ipo nafasi ya ngapi?
Katika mpambano wa mapema kati ya Tottenham na Arsenal umemalizika kwa Tottenham kushinda bao 2-1, magoli ya Tottenham yote mawili yamefungwa kipindi cha pili na Harry Kane dk 56 na dk 86,huku goli la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Meszuit Ozil dk 11. Hivyo Tottenham imepanda mpaka nafasi ya 5 na Arsenal kushuka hadi nafasi ya 6.

Mtanange mwingine ulioanza majira ya saa 12:00 jioni kati ya Astoni Villa na chelsea, Aston Villa ikiwa kwao villa park imejikuta ikilowanishwa 2-1, magoli ya chelsea yamefungwa na Eden Hazard dk 8 na Branslav Ivanovic dk 66 huku goli la kufutia machozi la Astoni Villa likifungwa na J.Okore dk 48. Hivyo chelsea inaendelea kujiimarisha kileleni kwa pointi saba mbele ya Man city wakati Aston villa ikikalia nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi.

Mchezo wa tatu ulikuwa kati ya Man city na Hull city ambapo Man city wakiwa nyumbani wamejikuta wakilazishwa sare ya 1-1, goli la Man city limefungwa na Milner dk 90+1 huku lile la Hull likifungwa na Meyler dk 35. Hivyo man city wakibakia nafasi ya pili na Hull nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi.

Palace ikiwa ugenini imeilaza Leicester 1-0,Bao la Palace limefungwa mnamo dk na hivyo Palace inashika nafasi ya  huku Leicester ikishikilia nafasi ya katika msimamo wa ligi hiyo

Watakatifu Southampton wameendelea kutafuta UEFA ilipo na leo wameshinda 1-0 mbele ya wenyeji wao QPR , bao la Southamptoni limefungwa na S.Mane dk 90+2 hivyo inashika nafasi ya 3 na QPR nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi hiyo.

Swansea wamelazimishwa sare ya 1-1 na Sunderland, goli la Swansea limefungwa na K. Sung-yueng dk 66
  na lile la Sunderland likifungwa na J Defoe dk 42 Hivyo Swansea inashikilia nafasi ya 9 na sunderland nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi
  • FT: Villa 1-2 Chelsea
  • FT: Man City 1-1 Hull
  • Chelsea seven points clear
  • FT: Leicester 0-1 Palace
  • FT: QPR 0-1 Southampton 
  • FT: Swansea 1-1 Sunderland
  • FT: Tottenham 2-1 Arsenal

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii