IVORY COST HAOO FAINALI AFCON
Timu
ya Ivory Coast imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika,
AFCON, baada ya kuilaza Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo 3-1 katika nusu
fainali ya
kwanza iliyochezwa Jumatano usiku katika mji wa Bata.
Alikuwa
nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure aliyeanza kuwanyanyua mashabiki wa
Ivory Coast alipofunga goli katika dakika ya 20 kutokana na mkwaju mkali
na kumwaacha mlinda mlago wa DR Congo, Kidiaba, asijue la kufanya.
DR Congo wakasawazisha bao hilo katika dakika ya 24 kwa njia ya penalti likifungwa na Mbokani Bezua.
Gervinho akafunga bao la pili katika dakika ya 41. Hivyo hadi mapumziko Ivory Coast ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi
cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana. Wilfried Kanon
alikamilisha sherehe kwa timu yake ya Ivory Coast alipofunga bao la tatu
katika dakika ya 68. Kwa matokeo hayo Ivory Coast imetinga fainali za
michuano ya Afcon mwaka 2015, ambapo inamsubiri mshindi wa nusu fainali
ya pili, kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea,leo hii
Nembo ya AFCON
Kikosi cha Ivory Cost
Maoni
Chapisha Maoni