HARRY REDKNAPP AJIUZULU LEO

Harry Redknapp amejiuzulu kazi ya kuifundisha timu ya Queens Park Rangers ya ligi kuu ya England,EPL.
Redknapp alimpigia simu mmiliki wa timu hiyo Tony Fernandes, siku ya
Jumanne akimweleza kujiuzulu kazi hiyo ya ukocha kutokana na sababu za kiafya.

Saa chache baada ya muda uliowekwa kumalizika, Redknapp alikuwa akimwaambia mtu ambaye alijenga imani kwake kama wiki mbili zilizopita kuwa kazi hiyo sasa basi.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67-alielezea matatizo yake ya kiafya kutokana na goti alilofanyiwa upasuaji kama sababu ya kuondoka kwake katika kazi hiyo lakini alionekana kuwa na thamani ndogo kwa kushindwa kuikwamua timu kutoka nafasi ya 19 iliyopo katika msimamo wa timu 20 za ligi kuu ya England.

 Harry Redknapp akishangilia baada ya timu yake ya QPR kupata bao


Harry Redknapp wakiongea na Luis Van Gaal kocha wa Manchester United


Haryy Redknapp alipokuwa QPR akifanyiwa Interview baada ya Mechi


 Harry Redknapp wakiteta jambo na Jose Mourinho kocha wa Chelsea baada ya mechi


Harry Redknapp akilia baada ya QPR kufungwa
 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii