BONY AMNYANG'ANYA NAMBA JOVETIC MAN CITY
Man
City imemuengua Mshambuliaji Stevan Jovetic katika kikosi
kinachoshiriki michuano ya klabu bigwa ulaya na nafasi yake kuchukuliwa
na
Wilfried Bony.Bony alisajiliwa na City mwezi uliopita akitokea Swansea City kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 25.
Uamuzi wa meneja Manuel Pellegrini kumuacha Jovetic unaamaanisha Man City itabaki na washambuliaji watatu wakubwa ambao ni Sergio Aguero Edin Dzeko na Wilfried Bony.
Jovetic, aliyekosa sehemu kubwa ya msimu uliopota sababu ya kuandamwa na majeraha ya nyama za paja amefunga jumla ya mabao 11 toka aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 22 toka Fiorentina mwaka 2013.
Maoni
Chapisha Maoni