BARCELONA USO KWA USO NA VILLARREAL COPA DEL REY

Barcelona watawakaribisha Villarreal wakati Athletic Bilbao watakutana na Espanyol katika hatua ya nusu fainali ya nusu fainali ya kombe la mfalme alimaarufu kama
Copa del Rey.
Barcelona v Villarreal
Tangu walipofungwa 1-0 na David Moyes' Real Sociedad mwanzoni mwa mwezi wa kwanza, Barcelona wameshinda jumla ya mechi 9 katika mashindano yote huku wakifanikiwa kutia wavuni jumla ya mabao 34.
Kuimarika kwa vigogo wa Catalan hao kumewafanya wapunguze gepu lililokuwa kubwa dhidi yao na Real Madrid na sasa ni pointi moja tu ili wawakute katika ligi ya  La Liga, lakini Luis Enrique amesema yeye amelenga sana kuchukua Copa del Rey ili aweze kujisafishia njia kwani yeye huu ni msimu wake wa kwanza.

Barcelona wanatakiwa kujua nini cha kufanya siku ya jumatano katika nusu fainali dhidi ya Villarreal, kwani walipokutana mwanzoni mwa mwezi huu Barca walijikuta wakichezea 3-2 mbele ya Enrique.

Villarreal wa kumuangalia kwa umakini ni winga Denis Cheryshev - ambaye anashika nafasi ya pili kwa kutoa pasi za mwisho La Liga (9) nyuma ya Lionel Messi - na mshambuliaji Luciano Vietto ambaye anajua kupiga mashuti kweli.

Barcelona, wao wanaamini kuwa Luis Suarez atawaangamiza Villarreal baada ya mshambuliaji huyo kufunga goli moja katika mechi tano ambalo alifunga jumapili dhidi ya Athletic Bilbao.


Barcelona v Villarreal

Februari 11, 2015, saa 6:55pm

 
 Suarez akifunga bao dhidi ya Athletico Bilbao

By Caunter Mgaya Jr.



 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii