ARSENAL YAAMBULIA KIPIGO EPL


Klabu ya Arsenal the gunners leo hii wameambulia kichapo cha bao 2-1 mbele ya wenyeji wao Tottenham katika mchezo uliochezwa mapema hii leo majira ya saa 10:00 za jioni ukiwa ni mchezo wa
raundi ya 24 ligi kuu Uingereza.

Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao mnamo dakika ya 11 kupitia kwa Mezuit Ozil ambapo mpaka mapumziko Arsenal walikuwa wanaongoza 1-0.

Katika mchezo ambao timu zote zilikuwa zikioneshana ufundi pamoja na kusaka magoli hali ilikuwa Tofauti kwa timu ya Arsenal katika kipindi cha pili ambapo waliruhusu mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wapinzani wao Totenham na kuwapa nafasi ya kusawazisha pamoja na kujipatia bao la ushindi.

Alikuwa ni HarryKane akiisawazishia Tottenham dakika ya 56 na kurudi tena wavuni kuipatia ushindi wa 2-1 timu yake mnamo dakika ya 86.

Hivyo Tottenham iliyokuwa nyuma ya Arsenal kwa pointi mbili kabla ya mchezo wa leo imefanikiwa kumshusha na kukalia nafasi ya nne kwa muda.


Wachezaji wa Arsenal wakishangilia bao lililofungwa na Ozil dk 11.

Meszuit Ozil akimtoka beki wa Tottenham.

.
Harry Kane akimtoka Beki wa Arsenal Atteta






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii