Ruka hadi kwenye maudhui makuu

LAMPARD APOKELEWA KIFALME STAMFORD BRIDGE

Frank Lampard Amefurahishwa na mapokezi ya shangwe kutoka kwa mashabiki wa Chelsea baada ya kurudi katika uwanja wa Stamford Bridge


Frank Lampard akiwapongeza mashabiki wa Chelsea baada ya mchezo kumalizika
 
Lampard akiwa upande wa Man City wamepata sare ya 1-1 dhidi ya vinara wa ligi kuu katika mchezo uliokuwa wa kasi kweli, Lampard akiwa kiungo aliingia mnamo dakika ya 77 akitokea benchi.
Lampard ambaye alimaliza msimu uliopita bila kujua kwamba ataweza kuondoka klabuni hapo jana alipagawishwa na shangwe za mashabiki wa Chelsea pamoja na mapokezi waliyo mpa kwa kuandika jumbe na mabango mbalimbali mengi yaki msifia na kusema hawato msahau.


 Frank Lampard wakiteta jambo na Branislav Ivanovic wa Chelsea


Lampard amesema: "Nimefurahishwa sana kwani kumekuwa na shangwe za kunipokea wakati nikiingia uwanjani kwa mashabiki wa pande zote mbili,upande wa Man City na wa Chelsea"
"Mashabiki wa Chelsea wamenitaka nirudi tena kwenye timu yao lakini sijui kilichotokea msimu uliopita mpaka nikaondoka. Nashukuru sana kwa kilichotokea"
Lampard anaamini pia kwamba Chelsea watakuwa wamefurahia pia na matokeo kwani wapo kileleni kwa pointi 5 mkononi mbele ya City. 

Mashabiki wa Chelsea wakimshangilia Frank Lampard hata kabla ya kuanza mechi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii