CHELSEA WALAMBA WINGA MPYA TOKA ITALY

Juan Cuadrado tayari amesha tua Chelsea, hayo yamebainishwa na kocha wa Fiorentina, Vincenzo Montella
Kocha huyo amesema kuwa Chelsea watafurahia huduma ya Juan Cuadrado.
Kwa mujibu wa viongozi wa Fiorentina ya
Italia; kijana huyo mkolombia mwenye umri wa miaka 26 bado yupo Italy, lakini ataondoka kwenda Uingereza jumamosi kwa kutumia ndege ya mtu binafsi saa moja asubuhi kwa ajili ya vipimo pale Stamford Bridge.
Fiorentina wanatarajia kupokea £23.33m kujumulisha na ofa ambayo watapewa Mohamed Salah kwa mkopo.

 Juan Cuadrado akiwa anasali kabla ya kuanza kucheza

 Juan Cuadrado akishangilia bao akiwa Fiorentina Italia


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii